Sandra - Msanii wa Bongo Movie
Akiongea ndani ya eNewz Sandra amesema watu wanaopata skendo mbaya kupitia umaarufu walioupata ndani ya bongo movie wanasababisha kupoteza heshima za wasanii wanaojiheshimu lakini pia inaharibu tasnia nzima ya bongo movie na kunyima ajira wasanii wengine.
Hata hivyo Sandra amewasihi na kuwashauri waandaaji wa bongo movie kuangalia watu wa kuwaweka katika movie lakini pia amewasihi wasanii wanaoingia katika tasinia wachague sehemu ambazo zinamfaa kuigiza ili kuweza kurudisha soko la bongo movie na kuwafurahisha mashabiki





