Jumapili , 6th Dec , 2015

Msanii wa muziki almaarufu kama Star 100 hivi sasa ameamua kuonesha kipaji chake tofauti na kazi zake kwa kumshirikisha nyota Belle 9 katika wimbo mpya uliobatizwa jina 'True Love' iliyofanyiwa kazi na mtayarishaji maarufu nchini Man Water .

Msanii wa muziki amabaye pia ni mjasiriamali almaarufu kama Star 100

Star 100 ameelezea nia ya kufanya kazi na mkali huyo anayeuwakilisha mkoa wa Morogoro akiweka wazi kuwa huu ni wimbo wake wa kwanza akielezea ugumu wake kumpata msanii kwa kushirikiana nae hadi kufikia hatua ya kumpata Belle 9 aliyeweza kuweka kiitikio katika wimbo wake huo.

Aidha star 100 mbaye licha ya kufanya muziki ni mjasiriamali mjini Moshi, ameendelea kusimama imara katika biashara zake na hapa anafafanua zaidi.