Ugonjwa uliopelekea kifo cha Mzee Matata

Jumatano , 16th Jun , 2021

Msanii wa maigizo ya vichekesho hapa nchini Tanzania Jumanne Alela maarufu kama Mzee Matata amefariki dunia jana saa 5:30 usiku katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alilazwa tangu 13.6.2021.

Picha ya Marehemu Mzee Matata enzi za uhai wake

Muigizaji mwenziye wa Tamthilia ya Mizengwe Mkwere original amesema Mzee Matata alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa muda mrefu na mpaka umauti unamkuta chanzo kilikuwa ni ugonjwa huohuo.

Mkwere Original amesema kwa mujibu wa familia ya Mzee Matata,  msiba upo Chamanzi kwa Mkongo na mazishi yatafanyika kesho saa 7:00 Mchana kwenye makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.