
wabunifu wa mitindo ya mavazi nchini Tanzania Twins Fashion
Twins Fashion ambao kwa mafanikio makubwa wamekwishawahi kufanya kazi ya kumvalisha msanii Diamond Platnumz na Makomandoo kati ya wengine, wamesema kuwa mitindo yao ambayo hubuni wenyewe, ina lengo la kuleta changamoto pia kwa wabunifu wengine ndani na nje ya Tanzania.
Wabunifu hawa pia wameiambia e-newz kuwa hivi sasa wameingia mkataba na msanii Jose Chameleone katika kazi ya kumtengenezea aina mbalimbali ya mitindo ya mavazi.
