Jumamosi , 4th Apr , 2015

Tunda Man, msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection ambaye hivi karibuni ameweka wazi mpango wake wa kuupa uhai zaidi muziki anaofanya kwa kuanzisha bendi.

Tunda Man

Tunda ametolea ufafanuzi suala hilo kupitia mahojiano yake na eNewz na kusema kuwa hatua hiyo ni baada ya kugundua kuwa muziki wa bendi ndio muziki wa ukweli zaidi.

Staa huyo ambaye amekuwa na mpango huo tokea mwanzoni mwa mwaka, amesema kuwa akishakamilisha mipango yote kuhusiana na hili, amejipanga kwaajili ya uzinduzi mkubwa ambao utahusisha kikamilifu timu ya EATV, kutokana na imani yake kubwa kwao katika usimamizi wa shughuli kama hizo.

Staa huyo amesema kuwa baada ya kuanza kwa bendi yake hii, mtu akimuhitaji kwaajili ya onesho, atatakiwa kumchukua na timu yake nzima, na atakuwa akifanya maonesho yake kama ambavyo anafanya sasa, na hatazingatia kuwa na sehemu maalum ambayo atakuwa akifanya onesho kila wiki kama ambavyo zinafanya bendi nyingi hapa nchini.