
Steve RnB
Akiongea kupitia eNewz Steve amesema kwa sasa ameshamaliza mkataba na uongozi aliokuwa nao hapo awali na yupo kwenye mazungumzo na uongozi mwingine na kwamba mambo yakikaa sawa atarudi tena kimuziki na kurudisha hadhi yake aliyokuwa nayo hapo nyuma.
Hata hivyo Steve amewaahidi mashabiki wake kwamba anajipanga kurudi upya ili kuwapa mashabiki zake ngoma kali na pia kutoa nyimbo mara kwa mara ili mashabiki zake wasimkose kwenye game.