Ijumaa , 2nd Nov , 2018

Video vixen, Amber Rutty pamoja na mpenzi wake ambaye jina lake halijajulikana, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam hii leo kwaajili ya kusomewa mashtaka juu ya kesi inayowakabili ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono mtandaoni.

Akiwa mahakamani hapo, Amber Rutty amesomewa mashtaka mawili, moja la kukubali kuingiliwa kinyume na maulimbe na kosa la pili ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono.

Wakati huo huo kijana anayejulikana kwa jina la James delicious naye amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka moja la kusambaza video za ngono mtandaoni, ambapo amekataa shtaka hilo.

Ifahamike kuwa iwapo watuhumiwa hao watakutwa na hatia juu ya makosa yao, kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watalazimika kwenda jela maisha au adhabu isiyopungua miaka  30 jela.