Ijumaa , 1st Jul , 2022

Rapa Billnass na Nandy wametoa taarifa ya kumchagua msanii wa filamu Steve Nyerere kuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi yao ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi huu wa saba.

Picha ya Steve Nyerere kushoto, kulia ni Billnass na Nandy

"Kamati ya harusi kwa kushirikiana na Bwana na Bibi Harusi tumemteua rasmi Steve Mengele ( Nyerere) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya harusi yetu" ameandika Billnass 

Wawili hao walichumbiana mwaka 2020 kisha wakarudia tena kuvalishana pete kwa mara ya pili siku ya Februari 20 mwaka huu 2022.