Jumamosi , 18th Apr , 2015

Stereo, Rapa mkali kabisa ambaye amerejea na ujio wa kishindo kupitia ngoma inayokwenda kwa jina Ukonga na Ilala aliyofanya akishirikiana na Chidi Beenz, amesema kuwa licha ya elimu aliyonayo, muziki kwa sehemu kubwa ndio unaoendesha maisha yake.

Stereo akiwa Studio

Stereo ambaye anashikilia Shahada ya Mipango Miji kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, pembeni ya fani yake hii, amesema kuwa, kwa sasa muziki ndio unaotangulia katika maisha yake kama anavyoeleza hapa.