Picha ya Roma na Stamina
“Kaka angu Stamina baadhi ya raia wanamkaanga sana wakimsema Uandishi wake (Word Play) kuwa ni wa kitoto. Binafsi napenda anachokifanya coz mbona tuna Rappers wengi tu wana Uandishi wao sio tu ni wa kitoto”
“But haueleweki yani hata ukimuuliza hapo ulitaka ku-Address nini hawezi kuwa na jibu coz haandiki uhalisia wowote yeye anachozingatia ni neno hili lina “Kina” fulani anatafuta lingine anasindikiza na neno linaloendana na kina hiko, hata kama sentesi haitaleta maana” - ameandika Roma
Roma na Stamina wanaunda kundi la ‘Rostam’ ambao tayari limetoa hits kibao kama Kijiwe Nongwa, Huku ama vile, Kaka tuchati, kaolewa, parapanda, hujambo mwanangu, sifa na kibamia.