Nuh ametoa kauli hiyo leo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, na kusema kwamba anayepaswa kutoa pongezi au kumtia moyo wa faraja ni mumewe Uchebe nasio yeye.
"Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na suala la Shilole kujenga nyumba. Mimi sitaki kuongea mambo ya Shishi halafu siwezi kumpa moyo kuhusu nyumba moyo atapewa na Uchebe sio mimi japo nilikuwa najua kuwa Shishi anajenga", amesema Nuh.
Kauli hizo za Nuh zimekuja ikiwa zimepita takribani siku nne tokea mwanadada Shilole, kuweka picha mtandaoni ikiwa inamuonyesha yupo katika harakati za kumaliza ujeizni wa nyumba hiyo.
Mbali na hilo, Nuh Mziwanda amefafanua kuwa sio kweli nyimbo yake aliyoitoa hivi karibuni amemshirikisha Ben Pol, bali kazi hiyo wamefanya wote pamoja kwa maana ni kazi yao wote.



