Msanii Juma Nature
Nature amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio na kusema kipindi walichokuwa wanafanya muziki enzi zao kulikuwa hakuna 'kiki' za kutengeneza ili nyimbo iweze ku-hit kama wanavyofanya wasanii wa kizazi kipya kutengeneza skendo fulani ili waweze kutengeneza wepesi wa kuachia ngoma zao ziwezeku-trend zaidi.
"Zamani unaimba 'Mic' inakupiga shoti ya umeme lakini unapaswa kuimba tu ili ushinde uweze kuingia disco Ijumaa. Mimi mwenyewe sijategemea kama ningekuwa 'Legendary' lakini mazoezi ndiyo yalinijenga, pamoja na kushindana sana. Tupewe fursa tu wakongwe maana watoto wa saizi wamepotea kidogo, wanaigana sana 'style' za zamani hakuna kuigana. Inabidi sisi wazee tuwaonyeshe", amesema Nature
Pamoja na hayo Nature amesema tamasha la 'Heshima ya bongo fleva' lilofanyika Julai mosi mwaka huu katika viwanja vya DAR LIVE kwa upande wake limekuwa la kihistoria kubwa katika maisha yake, kwani liliweza kumkutanisha na wakongwe wenzake ambao bado wanaonekana kuwa na uwezo wa hali ya juu katika muziki licha ya ukongwe wao.
"Binafsi nimependa kwa sababu nimekutana na rafiki zangu tuliyo-hustle muziki kitambo sana halafu ghafla hawapo lakini nilijisikia amani sana kukutana na wenzangu wa kitambo, mfano Dudubaya bado anauwezo na alichana vizuri na kuonekana wa kisasa", amesema Nature.
Mbali na hilo Juma Nature ametangaza ujio wake mpya katika muziki wa bongo fleva na ngoma mbili, wimbo mmoja ametengenezwa na P Funk Majani huku wimbo wa pili umetengenezwa na mtayarishaji Mr. T Touchez, hivyo anadai muda wowote ataziachia kazi hizo.


