.jpg?itok=6WV8We2s×tamp=1473272660)
Nahreel ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio, na kusema kuwa sababu alizopewa kwa kukatwa kwa kiashiria hicho hazikumridhisha.
“Sababu walizosema walisema tu stori ilivyoanza pale mbele ile slogan yangu ingeleta itilafu lakini it doesn't make sense, kwa hiyo ndo walitoa hiyo sababu lakini mimi niliona it doesn't make sense hata kama hiyo slogan ingekuwepo isingeharibu chochote”, alisema Nahreel
Kutokana na kitendo hicho Nahreel amewataka maproducer wengine kuitazama upya mikataba wanayoingia na wasanii, na iwapo wataenda kinyume na kutotumia slogan zao basi itakuwa wamekiuka mkataba.
“Kwanza sisi maproducer wenyewe tuwe strong kwenye hili suala, tukazie msanii anapokuja studio hizo slogan lazima kuweka hata na mkataba fulani kwamba hii slogan lazima iwepo, ukitoa hii kazi is no longer yours, kuwe na kitu fulani ambacho kinaweza kumbana msanii, kwa hiyo tuanze kuwabana wasanii hapa studio na kukubaliana kabisa”, alisema Nahreel.