Jumatatu , 5th Jan , 2015

Shishi Baby a.k.a Shilole, amesema kuwa, kwa upande wake mafanikio yake kimuziki yamekuwa yakichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuuchukulia muziki kama kazi ambayo ndiyo inaendesha maisha yake na familia yake.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini shilole

Shilole kwa nafasi yake amesema kuwa, siri ya mafanikio hususan kwa wasanii wa kike katika muziki ni kujituma, kufanya rekodi nyingi hata kama si kwaajili ya kuziachia akitolea mfano ya ngoma yake ya Malele kutoka badala ya rekodi nyingine 5 ambazo alikuwa amekwishazifanya.