Alhamisi , 18th Jun , 2015

Shilole ametangaza kumpa break mwenzi wake kwa muda wa mwezi huu mzima, wakitarajia kuendeleza malavi davi yao baada ya kipindi hiki kitakatifu kupita.

Shilole na Nuh Mziwanda

Kufuatia kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, wapenzi wanaoongoza katika vichwa vya habari vya Burudani kwa matukio mbali mbali, Shilole pamoja na Nuh Mziwanda wametoka na mpya baada ya Shilole kutangaza kumpa break mwenzi wake kwa muda wa mwezi huu mzima, wakitarajia kuendeleza malavi davi yao baada ya kipindi hiki kitakatifu kupita.

Kupitia mahojiano ambayo tumefanya na Shilole, staa huyo ameeleza kuwa kutokana na tofauti zao za imani, binafsi akiwa muislamu na Nuh akiwa mkristo, wanalazimika kufanya hivyo kutokana na mpenzi wake huyo kuwa hajakamilisha baadhi ya mambo ili kuweza kuwa naye kwa wakati huo.

Star huyo ameeleza juu ya wasiwasi wake endapo mwenzi wake huyo atachepuka katika kipindi cha likizo hiyo ya kuto kuduu kwa mwezi moja aliyompa ambapo amesisitiza kuwa anampenda sana 'baby' wake huyo.