Afande Sele pia kupitia mpango wa kuachia ngoma ngoma hii ambao utaambatana na show maalum kwaajili ya wapendanao katika siku hii muhimu kwao, amekuwa na ujumbe maalum wa upendo kwaajili ya mashabiki wake ambapo amewataka kutokupotosha maana ya Valentine Day.
Haya hivyo Afande pia aligusia swala la yeye na Mama Watoto wake (Mama Tunda) ambaye kwa sasa wametengana, ambapo amesema kuwa yeye na mwenzi wake huyu wa kipindi cha nyuma hawawezi kurudia tena enzi zao za pamoja kutokana na ukweli kuwa hakuna tena upendo uliokuwepo kati yao.