Alhamisi , 22nd Mei , 2014

Bendi maarufu ya muziki nchini Kenya Sauti Sol ambao wanafanya muziki wao kimataifa zaidi hivi sasa wanajiandaa kufanya ngoma mpya wakilishirikisha kundi nyota la muziki la nchini Afrika Kusini la Mi Casa.

Sauti Sol

Wakali hao kutoka Kenya wanaotamba na ngoma yao ‘Nishike’ wameweka wazi mpango huo mpya kupitia ukurasa wao wa twitter wakiwasihi mashabiki wao kuwa wakae mkao wa kula kwa ngoma hiyo kali.

Sauti Sol imekuwa ni moja ya bendi maarufu barani Afrika ambayo imesimama imara kwa muda mrefu na kufanya matamasha mbalimbali ya kimataifa.