Jumatatu , 30th Dec , 2019

Mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya muziki wa HipHop nchini, Rosa Ree,amejitaja kuwa ndiye mwanamke bora wa mwaka kwa upande wake, kutokana na mengi mazuri aliyoyafanya ndani ya mwaka 2019.

Msanii wa HipHop nchini Rosa Ree.

Rosa Ree ameieleza EATV & EA Radio Digital, kuwa kuna mambo mengi ameyafanya ikiwemo kujiamini, kuachia kazi mara kwa mara na kwenda Kimataifa na kwamba anayo mipango ya kuachia Album.

"Mwanamke wa mwaka kwangu ni Rosa Ree, kwa sababu sijui wanawake wengine wanapitia nini ila ninachojua kuhusu mimi vile ninavyopitia, vitu ambavyo nimeweza kuvipita na kuvikimbiza kwa mwaka 2019, pia najua uzoefu wangu peke yangu na sijui kuhusu watu wengine wamefika vipi walipofika" ameeleza Rosa Ree.

Msanii huyo ameendelea kusema "Changamoto ambayo nakutana nayo kila siku na kupambana nayo ni kukata tamaa, kwahiyo siwezi kutaja wengine ila mwanamke wa mwaka ni Rosa Ree, na mwanamke wa maisha yangu yote ni mama yangu" ameongeza.