Jumatano , 1st Dec , 2021

Wanasayansi kutoka chuo cha Vermont, chuo cha Tufts na taasisi ya baiolojia ya Wyss wamegundua kuwa cell za xenobots zikikusanywa pamoja zinaweza kuunda roboti nyingine mpya.

Picha ya mfano wa robot

Xenobots ni roboti iliyoundwa na mtaalamu wa computer na maroboti Professor Josh Bongard kutoka chuo cha Vermont kwa kutumia chura kutoka barani Afrika. Roboti hii mpaka sasa bado ni cell inayoishi maabara na itakua tofauti na maroboti mengine yaliyoundwa kwa kutumia chuma.