Jumamosi , 3rd Mei , 2014

Msanii wa muziki wa injili wa nchini Kenya, Ringtone kutoka katika ziara aliyoifanya huko Nigeria, ameweza kukutana na kiongozi wa kanisa la Revival Assembly la Pasta Anselm Madubuko, ambaye ni mume wa msanii Emmy Kosgei kutoka nchini Kenya.

Ringtone

Ringtone amesema kuwa, ameweza kupata wakati mzuri pamoja na kiongozi huyu wa kanisa, ingawa hakuweza kukutana na Emmy ambaye bado yupo huko Marekani kwa ziara ya kimuziki.

Ringtone ameweka wazi kuwa amefanikiwa pia kufanya kolabo na wasanii kutoka nchini humo, akiwepo Nikki Laoye, Innerman na Provabs ambao wanafanya vizuri sana kupitia muziki wanaoufanya huko Nigeria.

Tags: