Jumapili , 20th Nov , 2022

Msanii Rayvanny na Zuchu kutoka Tanzania wameshinda tuzo za AFRIMMA 2022 katika vipengele vya msanii bora wa kiume Africa Mashariki na msanii bora wa kike Africa Mashariki.

Picha ya Rayvanny na Zuchu

Katika kipengele cha msanii bora wa kiume Africa Mashariki Rayvanny amewapiga chini wasanii Diamond Platnumz, John Frog - South Sudan, Khaligraph Jones - Kenya, Eddy Kenzo - Uganda, Otile Brown – Kenya, Meddy – Rwanda na Sat B - Burundi.

Kwa upande wa msanii bora wa kike Africa Mashariki Zuchu amewashinda  Maua Sama, Nandy, Femi One, Sanaipei Tande na Jovial kutoka Kenya, Sheebah Karungi na Winnie Nwagi wa Uganda.