Jumapili , 22nd Feb , 2015

Msanii wa muziki Ras Six, akiwa kama moja ya wanaharakati wa kutetea haki za walemavu hususan watu wenye Albinisim, yeye mwenyewe akiwa mmoja wao, amelaani mauaji yanayoendelea dhidi ya albino.

Ras Six

Amesema kuwa kuna umuhimu wa vyombo vya habari na vyombo vya usalama kuwahusisha zaidi katika vita vya kupambana na ukatili huo dhidi yao.

Ras Six amesema kuwa, kushirikishwa kwao zaidi katika vita hiyo kutaongeza nguvu kutokana na wao kuguswa moja kwa moja na tatizo hilo na kuweza kulielezea kwa undani zaidi, na vilevile msanii huyo akatumia nafasi hii kulaani mauaji ya albino yaliyotokea hivi karibuni huko kanda ya ziwa.