Ijumaa , 5th Dec , 2014

Rapa Wangechi ambaye alipata ajali mbaya ya gari mwezi Septemba mwaka huu, ameendelea kupata nafuu ambapo kwa sasa anaendelea na baadhi ya mazoezi ya viungo kwa wataalam wa physiotherapy kwa ajili ya kurejesha hali ya kawaida.

msanii wa miondoko ya rap nchini Kenya Wangechi

Rapa huyu kwa njia ya mtandao amewafahamisha mashabiki wake juu ya kurejea kwa uwezo wa kufanya kazi wa mkono wake wa kushoto baada ya matibabu haya.

Wangechi ameendelea kutumia mitandao ya kijamii kuwapa mashabiki wake taarifa za maendeleo ya afya yake, akiwa tayari anaendelea na mazoezi ya kutembea, na pia kukiwa na taarifa za matumaini makubwa juu ya maendeleo yake kutoka kwa watu ambao wamepata nafasi ya kumtembelea na kumuona kwa macho.