Jumanne , 7th Jun , 2016

Msanii Nyauloso amefunguka kuhusu kolabo yake aliyofanya na Q Chilla ya Aza, na kusema kuwa wimbo huo ulisababisha Q Chief kutoa chozi.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Nyauloso amesema siku hiyo walienda studio kurekodi, lakini baada ya Qchief kuisikia beat hiyo, alipata hisia kali zilizopelekea kutoa machozi.

“Nakumbuka wakati nataka kufanya kazi na Q Chief nilimfuataga kwanza Mbezi (producer) tukaja mpaka studio tukaanza kufanya kazi, lakini baada ya kupiga ile beat yetu akasikiliza sikiliza akawa kama mood hana, akaenda nje akavuta sigara akaja, akaweka hilo beat la Aza la zouk, huweiz amini Q Chief alikuwa anatikisa kichwa kwa hisia mpaka machozi yanamtoka, akaniambia hii ndo nyimboambayo tunatakiwa mimi na wewe tufanye”, alisema Nyauloso.

Baada ya tukio hilo Nyaulose aliendelea kusema kuwa Q Chief akaandika chorus yake na kuipiga pale pale, na kumuacha yeye akiwa hajaingiza verse yake, na kuja kuifanya siku nyingine.