Jumanne , 3rd Nov , 2015

Star mkongwe wa muziki wa rap ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Mikumi, Professor Jay ametoa wito kwa vijana kujituma na kuwa chachu ya kufanya mabadiliko katika taifa lao, hatua ambayo wanatakiwa kuichukua sasa bila kujali itikadi za vyama vyao.

Staa mkongwe wa muziki wa rap na Mbunge mteule wa Jimbo la Mikumi, Professor Jay

Professa Jay ameeleza kuwa, kijana yoyote anayeona ana uwezo wa kufanya mabadiliko anatakiwa kufahamu kuwa siasa imeisha na mabadiliko kuyavuta maendeleo ndiyo kitu cha msingi zaidi, na hii si kwa watu wa Mikumi pekee, bali ni kwa taifa zima.

Kuhusiana na maneno haya ya busara, huyu hapa Professa Jay mwenyewe anaeleza.