Ijumaa , 6th Nov , 2015

Baba wa muziki wa rap hapa Bongo, Professor Jay baada ya kuwatoa wasiwasi mashabiki wake kuwa nafasi aliyoipata sasa kisiasa nchini haiwezi kumuondoa katika gemu ya muziki.

Staa wa muziki wa rap hapa Bongo Professor Jay

Star huyo ameeleza kuwa nafasi hiyo zaidi itakuza nafasi yake kimuziki ambapo sasa atakuwa akiufanya katika ngazi kubwa zaidi na kufungua milango mingine.

Proffesor Jay ameeleza kuwa, anatarajia kufanya muziki bora zaidi na kolabo na wasanii wakubwa kabisa, akimtaja kwenye mpango star mkubwa kama Eminem na Jay Z, muziki ambao kwa maneno yake binafsi amesema utakuwa ni katika next level bila kusahau kuwatumikia wananchi wake wa Mikumi.