Vanessa Mdee akionyesha jina la Rotimi kwenye kifua chake
Kupitia video ambazo zimetawala kwenye mitandao ya kijamii zimewaonesha kila mmoja kumchora Tattoo mwenzake ikiwa kama ni ishara ya upendo, urembo na kumbukumbu kwenye mahusiano yao.
Rotimi amesema ana michoro mingi kwenye mwili wake ikiemo ya picha ya Yesu, 'Ego', Simba na sehemu ya peponi, pia akaongeza kusema ana tattoo yenye jina la Vanessa Mdee mkononi mwake.
Aidha kwa upande wa Vanessa Mdee yeye akaonesha tattoo yenye jina la Rotimi ambayo ameichora maeneo ya kifuani mwake.
Siku kadhaa zijazo wawili hao wanatarajia kutimiza mwaka mmoja tangu walipoanzisha mahusiano yao mwezi Oktoba 2019.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.