Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Rapa Octopizzo kutoka nchini Kenya ameendelea kutumia nafasi yake kama msanii kumulika changamoto ambazo wakimbizi wanakabiliana nazo katika kambi zao, hususan huko nchini Kenya akiwa balozi wa mahusiano mema kutetea haki za wakimbizi chini ya UNHCR.

Octopizzo

Msanii huyu ametoa ujumbe wake kwa mashabiki zake kwa jamii na mashabiki kwa ujumla kutokusahau kuwa wakimbizi ni watu waliotoka katika maisha na hali za kawaida kama mtu mwingine yoyote yule, na hali yao ya ukimbizi haikuwafika kwa kuchagua.

Staa huyo kupitia nafasi yake anaendeleza mradi unaofahamika kama “Artistes for Refugees” kusaidia wakimbizi hawa kufikia ndoto zao kupitia fani na vipaji mbalimbali walivyonavyo.