Jumatano , 11th Jun , 2014

Rapa Octopizzo amechaguliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi, UNHCR nchini Kenya, kutoa burudani pamoja na kuzungumza na wakimbizi hao katika kambi za Daadab na Kakuma.

Rapa Octopizzo akipanda ndege

Octopizzo amesema kuwa maadhimisho hayo yatakayofanyika siku ya Wakimbizi Duniani tarehe 20 mwezi huu yamempa furaha kupata nafasi hii, huku akitaka wakenya kujivunia kutoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi laki 4 wanaoishi nchini humo, na kila mmoja kutumia nafasi yake kusaidia jitihada za shirika la UNHCR Kenya.

Rapa huyu mwenye mafanikio ametumia nafasi hii kutoa wito kwa mashabiki wake kuishi katika mtindo wa maisha ambao unakidhi mahitaji yote ya maisha yenye manufaa kwa mtu binafsi pamoja na wale wanaomzunguka.