
Octopizzo amesema kuwa, katika nafasi hii, changamoto yake kubwa imekuwa ni muda wa kukaa karibu na kuwapa malezi watoto hawa, kutokana na kazi yake ya usanii kumuweka safarini kila wakati.
Rapa huyu ameweka wazi pia kuwa, suala la yeye kutambulika kama Octopizzo bado ni kitendawili kwa watoto wake ambao bado wanaelewa kidogo kazi yake, na sasa msanii huyu amesema kuwa anajifunza kuweka umuhimu katika baadhi ya mambo yanayomhusu, ikiwepo familia yake.