msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Kenya Octopizzo akiwa na mwanae Tracy
Octopizzo mwenye watoto wawili wa kike ameonesha kila dalili za kuthamini mchango wake katika kumpa elimu mwanaye huyo wa kwanza licha ya muziki wake kuchukua muda mwingi katika kazi zake za kila siku.
Rapa huyo aliyekulia katika mazingira duni ya huko Kibera amemshukuru mwanaye kuweza kuhitimu masomo yake katika shule ya awali na ataendelea kumsapoti kila siku ili aweze kufikia malengo ya maisha yake ya baadaye.