Jumamosi , 10th Nov , 2018

Msanii wa kike wa muziki wa nchini Kenya, Nyota Ndogo, ametoa ruhusa kwa mtu yeyote kumshikisha adabu mtoto wake wa kike Barka, iwapo atamkuta anafanya maovu.

Nyota Ndogo ametoa ujumbe huo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kusema kwamba iwapo mtu atamuona binti yake amebananishwa na mwanaume, asimuache aendelee kufanya hayo na badala yake amchape ili kumpa fundisho, kwani watoto ni wa wote.

“Mukimuona Barka amekua mkubwa, umkute amebanwa ukutani na mwanamume ama kijana na amevaa nguo za shule chukua fimbo tandika huku ukimuuliza kwenu wapi, mlete nyumbani kwangu ukimwambia maisha magumu sana kwanini unataka kuyaharibu”, ameandika Nyota Ndogo. 

Nyota Ndogo ameendelea kwa kusema kwamba ni vyema kuzungumza na watoto na kuwaonya, pia wazazi washirikiane katika malezi kwani hata kama sio wako wa kumzaa.

Nyota Ndogo akiwa na binti yake Barka.