Jumanne , 18th Feb , 2014

March 8, inatarajiwa kuwa ni siku ya kipekee nchini Uganda kutokana na maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo yatapambwa vizuri kabisa na msanii wa muziki wa kimataifa, Nyanda kutoka huko nchini Jamaica.

Katika tamasha hili la aina yake, Nyanda anatarajiwa kupashiwa jukwaa na wasanii wakali kabisa wa nchini Uganda akiwepo Keko, GNL Zamba, Cindy na wengine wakali.

Nyanda ni kati ya wasanii waliojipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki akiwa na mwenzake Nailah ambao kwa pamoja walikuwa wanaunda kundi mahiri la Brick n' Lace.