Alhamisi , 2nd Apr , 2015

Mchekeshaji maarufu wa nchini Kenya Eric Omondi amezidi kukamata vichwa vya habari baada ya kufanya ngoma aliyoitumia midundo ya wimbo wa msanii Diamond Platnumz ‘Number one’ na kuvunja mbavu watu kwa jinsi alivyoiga na kuweka mashairi yake binafsi.

Mchekeshaji maarufu wa nchini Kenya Eric Omondi

Omondi ambaye kwa sasa amejikita katika kufanya ziara za matamasha yake ya vichekesho amefurahi kuona video hiyo imepokelewa vizuri na mashabiki katika ziara yake nchini Marekani huku akijipanga kufanya tamasha la sikukuu ya Pasaka maalum la kuwasaidia watoto wasiojiweza wafurahie Sikukuu hiyo.

Kichupa hicho kipya 'Rafiki Pesa' kimefanyiwa shooting nchini Kenya kikishirikisha wasanii Chipukeezy, Owago Onyiro na David The Student na wengineo wengi.