Jumatano , 11th Nov , 2015

Msanii Nuh Mziwanda ameweka wazi kuwa, katika safari yake ya muziki baada ya kusimama kama msanii binafsi, aliwahi kushawishiwa kuingia katika biashara ya dawa za kulevya na baadhi ya mabosi ambao aliwafuata kuwaomba msaada kuendesha muziki wake.

Nuh Mziwanda

Nuh amesema kuwa, kutokana na malengo aliyokuwa nayo katika muziki huu, aliweza kuvuka kishawishi hiki akiwa ana amini kuwa asingeweza kusimama mpaka sasa kama msanii, endapo anayeingia mkenge na kuanza kufanya biashara hiyo.