Jumamosi , 6th Jun , 2015

Utata kuhusiana na sakata zima la taarifa za Nuh Mziwanda kumtia mimba mchepuko, na kusababisha vita kali kati yake na Shilole ambaye ni mpenzi wake, limepatiwa ufumbuzi usiku wa jana katika show kali ya burudani ya Friday Night Live.

Nuh Mziwanda na Shilole

Kama ulipitwa, picha zima kuhusiana na sakata hili lilianza kwa Nuh kutolea ufafanuzi kashfa hiyo inayomkabili, akidai anampenda sana Shishi wake.

Baada ya Nuh kusepa, exclusively FNL wakamleta mbele ya Afrika Mashariki Rose, Mchepuko aliyedai kuwa na mimba ya msanii huyo ambaye licha ya kupotezea suala zima la kuwa na ujauzito, ambapo alikana kuwa na mimba ya msanii huyo, lakini kukiri kuwa anampenda na wamewahi kukutana kimwili, "ku-do", ama kufanya mapenzi katika siku za hivi karibuni bila ya Shilole kujua.

Picha halikuishia hapo, Maelezo haya yakamfanya Shilole kutoka huko alipokuwa na kumchukua Nuh na kurejea naye katika show, uso kwa uso na mchepuko wa baby wake, Rose ambaye mbele ya Afrika Mashariki na mbele ya Nuh na Shilole akasema kuwa suala la kutangaza kuwa ana mimba ni la uongo na alisema kwa hasira baada ya Shilole kumshambulia na kumuumiza baada ya kumkuta akiwa karibu na Nuh Mziwanda, na baada ya hapo kuwaomba radhi wapenzi hao kwa usumbufu aliowasababishia.

Usikose kusikia mahojiano ya kipekee kati ya Nuh na eNewz wiki ijayo kusikia amejipanga vipi na Shilole kupata mtoto wao hasa baada ya kukabiliana na msukosuko wa mimba ya kusingiziwa.