Jumanne , 13th Mei , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nikki wa Pilli leo hii ametambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Sitaki Kazi ambayo amemshirikisha ndani yake msanii Ben Pol pamoja na G Nako.

Nikki wa Pilli amesema kuwa, kazi hii ni kwaajili ya kuwahamasisha vijana kujishughulisha wenyewe kujipatia kipato na kuacha kutegemea kuajiriwa, huku akiwashauri wale wenye elimu ya juu kutengeneza fursa za ajira kwa wengine.

Nikki wa Pilli amesema kuwa, yeye kwa upande wake akiwa kama msomi ameanzisha taasisi ambayo itakuwa inasaidia kuwafungua vijana macho na kuwaonyesha njia za mafanikio, mpango ambao atafafanua zaidi juu yake hivi karibuni.