Nikki wa Pili
Nikki amesema kuwa taasisi hii imejikita katika kutumia sanaa na media katika kuongeza kasi ya maendeleo, ikiwa na Klabu mbalimbali ndani yake, Twaonekana Media Club, Twaonekana Jamii na Twaonekana Watoto ambayo imelenga kuwajengea watoto sauti ya kusema mambo yao katika jamii.
Katika mahojiano haya, Nikki pia akazungumzia swala la Weusi Mtu Tano, na kwanini kwa sasa wanashine zaidi wakiwa watatu tu, ambapo amesema mara nyingi Bonta ambaye ni moja ya wasanii ndani ya Kundi amekuwa akibanwa na shughuli zake za udaktari, wakati Lord Eyes akiwa Studio akiandaa kazi mpya ambazo zitatoka sambamba na taarifa ya kurejea kwake kundini.