Jumanne , 1st Apr , 2014

Jose Chameleone anatarajiwa kupiga hatua nyingine kubwa katika muziki wake, kwa kufanya kolabo na wasanii wa muziki wa Kimataifa akiwepo Sean Paul pamoja na Konshens kutoka nchini Jamaica.

Chameleone

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa, wasanii hawa wameamua kumchagua Chameleone kutoka Afrika Mashariki baada ya kuona jitihada na uwezo mkubwa wa msanii huyu katika muziki wake ambao unakuwa siku hadi siku.

Ujio wa kazi hii kali unakwenda sambamba na ujio wa kazi mpya za kiwango cha juu kabisa kutoka kwa Jose Chameleone kwa mwaka huu, ikiwepo rekodi pamoja na video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina 'Gimme Gimme'.