Ijumaa , 7th Mei , 2021

Msanii wa Taarab Isha Mashauzi amesema yeye na aliyekuwa mume wake walikutana Visiwani Zanzibar lakini kitendo cha kuvunjika kwa ndoa yao amekitafsiri kama haikua riziki yake kwa sababu alimpenda sana mume pamoja na mtoto wake.

Msanii Isha Mashauzi

Isha Mashauzi amesema alikutana na mume wake huyo huko Zanzibar baada ya kufukuzwa nyumbani kwao na mama yake mzazi

"Nilifukuzwa nyumbani na mama baada ya kukutwa na rafiki yangu aliyekuwa amelewa,nikaenda kuishi Zanzibar, huko nilimpata baba mtoto wangu na baada ya hapo ndiyo ikabidi nirudi nyumbani tena kwa ajili ya ndoa, ngawa ndoa haikua riziki"

"Nilivyoolewa ndoa ya pili, nilikuwa nampenda sana mtoto wa mume wangu na mpaka sasa hivi ameolewa, nilimlea kwa misingi niliyofundishwa mimi" ameeleza Isha Mashauzi