Jumatatu , 24th Feb , 2014

Navy Kenzo, kundi la muziki ambalo kwa sasa linatikisa chati mbalimbali kwa ngoma yao ya Chelewa na mtindo wa dansi wa Bokodo, wamekutana na eNewz kupiga stori mbalimbali ikiwepo kueleza mipango yao mikubwa kwa mwaka 2014.

Navy Kenzo ikiwa ina maana ya Jeshi ya watu watatu, wamesema kuwa wana mambo makubwa ambayo wameandaa kwa ajili ya mashabiki wao baada ya kuona mapokezi mazuri ya singo ya Chelewa ambayo imewapa msukumo wa kufanya kazi bora zaidi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Vilevile kundi hili linalounda na Nahreel, Aika pamoja na Weestar wameongelea juu ya video yao ya ngoma ya Chelewa ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa mitaani ambapo wamesema kuwa, matayarisho yamekwishakamilika na muongozaji Adam Juma ndiye atakayeifanya na hivi karibuni itatoka kwaajili ya wapenzi wa muziki.

Navy Kenzo wamesisitiza kuwa kutokana na mfumo wa Uhuru mkubwa uliopo katika kundi lao, wana uhakika wa kudumu kwa miaka mingi bila kutengana kama makundi mengine, ambapo wataendelea kutengeneza kazi nzuri na bora zaidi kwaajili ya mashabiki wao ambao wameongezeka kwa kasi kubwa.