Jumatano , 26th Mei , 2021

Mtoto wa Mama Saidi Chege Chigunda amemtaja msanii Juma Nature kama ndio Mfalme wa muziki wa BongoFlava kwa sababu ya uwepo wake na kuacha alama kwenye muziki.

Juma Nature kulia na Chege Chigunda kushoto ndani ya East Africa Radio

Akizungumzia hilo kwenye show ya PlanetBongo ya East Africa Radio, Chege amesema hakuna mtu yeyote anayebisha suala hilo kwamba Juma Nature ndio Mfalme wa BongoFlava.

"Nia ya kumuweka Nature aonekane vile kwenye video nilitaka kuacha alama kwa kuwa Juma Nature ni Mfalme kwenye muziki wa BongoFlava na hakuna mtu yeyote anayeweza kubisha, brother kaacha alama kubwa sana kwenye muziki huu" ameeleza Chege

Wawili hao wameungana tena baada ya kuwa na tofauti za kibiashara kwa kipindi cha muda kirefu na wameachia kazi yao mpya ya kucha.