Jumanne , 6th Jul , 2021

Unaambiwa Recho Kizunguzungu haelewi kitu kuhusu wanaume wahuni, warefu, na weupe kwani anawaelewa kinoma na ndiyo wanaume ambao ana-enjoy nao akiwa kwenye mahusiano.

Msanii Recho Kizunguzungu kwenye studio ya East Africa Radio

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Recho Kizunguzungu anasema utofauti wa wanaume wa kawaida na wahuni anaowapenda yeye anaujua mwenyewe wakiwa kwenye mahusiano na hawezi kumwambia mtu yeyote.

"Sijawahi kupenda mwanaume mweusi, napenda wanaume weupe, warefu, wawe wahuni wahuni fulani hivi, utofauti wao naweza kuujua mwenyewe kipindi ninapokuwa naye huko ndani, hizo sifa siwezi kumwambia mtu yeyote kwa hiyo sifa zao ninazo mimi mwenyewe na na-enjoy kumuona" amesema Recho Kizunguzungu

Mengine zaidi kuhusu sifa za mwanaume anayemtaka mtazame hapo chini akimzungumzia.