
Nandy
Mrembo huyo amesema kuwa amefungua kampuni yake binafsi inayojihusisha na utengenezaji wa nguo za kitenge, mikoba, nguo za harusi pamoja na mavazi mengine ya utamaduni inayojulikana kwa jina la Nandy African Print.
"Nilianza ujasiriamali tokea nipo chuo kabla masuala ya muziki hayajachanganya vizuri nilikuwa naenda kununua nguo Kariakoo halafu ninazipamba vizuri kwa kutumia vitu vya asili". Alisema Nandy
Aidha msanii huyo amesema mpaka sasa ameweza kutoa ajira kwa watu watano ambao ni mafundi wanajishughulisha na utengenezaji wa nguo za asili yaani mafundi cherehani.
"Sijakurupuka kufungua kampuni yangu kwani nilijipanga muda mrefu tokea kipindi ninashiriki mashindano ya muziki nchini 'Nigeria' nikasema nikishinda lazima nitimize lengo langu la muda mrefu, nilianzia na mtaji wa milioni 10 kwa ajili ya kununulia vifaa pamoja na kulipia kodi". Alisema msanii huyo
Kwa upande mwingine msanii huyo alisema malengo ya kampuni yake ni kuhudumia ndani na nje ya nchi kwa kutoa mavazi ya asili yenye ubora zaidi.