Jumanne , 23rd Jun , 2015

Mtayarishaji muziki na msanii kutoka kundi la Navy Kenzo, Nahreel Mkono ameweka wazi kuwa Weestar, staa aliyekuwa katika kundi hilo kipindi cha nyuma, alikuwa ni mpango makusudi kufuta mtazamo wa mahusiano ya kimapenzi kati yake Haika.

Navy Kenzo

Nahreel ameeleza kuwa, mbali na kipaji cha msanii huyo, alikuwa ni kwa ajili ya kusaidi Navy Kenzo kuonekana kama kundi zaidi na si muunganiko wa wapenzi, kitu ambacho baadaye waliamua kuachana nacho baada ya kuona kuwa kuna baadhi ya mambo yanashindwa kwenda sawa pamoja na msanii huyo.

Nahreel bila kueleza sababu hasa za kusitisha kufanya kazi na Weestar kama kundi ameeleza kuwa, wao ndio waliomshauri staa huyo kusimama kama solo artist huku ukaribu, urafiki na utayari wao kuendelea kufanya kazi pamoja ukiwa pale pale.