Jumanne , 18th Apr , 2017

Msanii AT ametunga wimbo maalum ambao ameupa jina la 'Nahama' huku kwenye wimbo huo akielezea mambo mengi ambayo yanampelekea kuhama katika jiji hilo la Dar es Salaam likiwemo sakata la kutekwa kwa Roma Mkatoliki.

AT

Katika wimbo huo wa AT ameanza kumshukuru mama yake mzazi ambaye amekuwa akimshauri kutokukaa kimya katika baadhi ya vitu vinavyoendelea nchini bali amekuwa akimshauri ajaribu tu kutumia maneno yenye staha ili mabaya yasiweze kumkuta.

Wimbo huu wa AT baadhi ya mashabiki wameuhusisha na masuala ya siasa yanayoendele nchini hivi sasa. Isikilize na kuitazama kazi hii hapa