Nikki Mbishi ameyasema hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika waraka wa kulalamikia mfumo huo, na kudai kuwa utafiti alioufanya unaonesha kuwa kuna baadhi ya watu wanaosimamia wasanii wanafanya hivyo kwa kujuana.
“Obviously kwa utafiti wangu mdogo naweza kusema muziki wetu wa Tz unakufa gradually na wale wanaojiita wadau wanajua hilo, muziki umekuwa kama kitu cha kifamilia, yaani kama sio mwanafamilia kupata nafasi kwenye nyanja yoyote itabaki ndoto kwenye career yako hata uwe una uwezo wa Nabii Mussa”, aliandika Nikki Mbishi.
Nikki Mbishi aliendelea kwa kusema kuwa iwapo watu hao wameweza kuwatangaza wasanii watano wakafika kimataifa, inakuwaje washindwe kuwatangaza na wengine kutokana na misingi ambayo tayari wameshaweka, na hatimaye kukuza muziki.
“Huwa najiuliza hivi, kama wadau wameweza kuwa brand wasanii watano Tanzania nzima wakafika hatua fulani kisanaa, kwanini wanashindwa kubrand wasanii 100 ambapo uwezo huo wanao kupitia patnerships zao walizonazo na makampuni makubwa”, alisema Nikki Mbishi.
Nikki Mbishi aliendelea kwa kusema kuwa muziki wa Tanzania umelaaniwa kutokana na mfumo uliopo, na watu kutumia fursa kujinufaisha wenyewe na kukandamiza.
“Tanzania imelaaniwa kwenye sekta ya sanaa, michezo na burudani, wanaojiita wadau hawana hata aibu kujifanya wanajivunia mafanikio, msanii gani Tanzania amesainiwa na Label kubwa duniani ukimtoa Rose Mhando? Tanzania ni kujuana kwingi kuliko kuweka professions mbele, kila fursa inatumika kunufaisha wachache na kukandamiza wengi”, alisema Nikki Mbishi kwenye maneno yake aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.