Mwimbaji wa bendi ya Kalunde nchini Tanzania, Deborah Nyangi
Deborah amegundua kuwa mwanae anayeitwa Florence Florenso siku zote ambazo anakuwa akimlea anaonyesha kuwa ana kipaji cha kupiga kinanda kitu ambacho kinamvutia mtoto huyo.
Aidha Deborah anayefanya vyema kwa kutoa video yake inayotamba hivi sasa katika stesheni mbalimbali nchini iliyobatizwa jina "Fingo', ameongezea kuwa anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayopikwa na prodyuza C 9, huku akijianda kutoa albamu yake mpya itakayowashirikisha wanamuziki mbalimbali nchini.





