Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira N. Maregesi
Akizungumza na makundi yaliyofuzu hatua ya fainali Jijini Dar es Salaam Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira N. Maregesi amesema sanaa ni ajira na BASATA kama msimamizi wa shughuli za sanaa wameona ni vyema wakashiriki kikamilifu katika hatua zote za shindano ili kuona haki inatendeka.
“Kundi litashinda kutokana na namna litakavyoonesha ubunifu pamoja na mambo ambayo mmeelekezwa na majaji na katika makubaliano yenu ya ushiriki, hivyo hakuna kundi litakalopendelewa, haki itatendeka hivyo kajiandaeni kwa hari mkijua mshindi atapatikana kadri ya kazi atakayoonyesha” Amesema Maregesi wakati akiyapa maelekezo makundi
Shindano la Dance100% linaendeshwa na EATV na kudhaminiwa na VODACOM na COCA -COLA na kuonyeshwa na EATV kila Jumapili saa moja jioni.