Jumanne , 1st Apr , 2014

Wasanii wa muziki hapa Bongo, Peter Msechu kwa kushirikiana na msanii Mrisho Mpoto wameamua kuungana pamoja na kutengeneza kazi inatokwenda kwa jina 'Usiniue Nitunze',.

Peter Msechu

Kazi hii pia ni kampeni kwa ajili ya kupambana na suala zima la Ujangili ambalo linatishia kupotea kwa wanyama Tembo ambao ni rasilimali kuwa na kivutio cha utalii hapa nchini.

Msechu ambaye ameongea na eNewz kwa kirefu kuhusiana na mpango huu, amesema kuwa wazo hili lilimjia baada ya kuona vitendo vya ujangili vikizidi, huku waathirika wenyewe wanyama Tembo na Faru wakiwa hawana uwezo wa kusema wala kujitetea, kitu ambacho kilimpa msukumo yeye kama msanii kusimama mstari wa mbele kuwasemea wanyama hawa.